July 13, 2019

NYOTA wa Simba, Marcel Kaheza kwa sasa yupo kwenye hatua za mwisho kujiunga kwenye kikosi cha Tanzania Prisons.

Kaheza amemalizana na AFC Leopards ya Kenya alikokuwa anakipiga kwa mkopo kwa sasa yupo Dar habari zimeeleza kuwa anawinwa na Prisnons.

Mmoja wa kiongozi wa Tanzania Prisons amesema kuwa walianza kufanya mazungumzo na Kaheza kabla ya kutua Simba akitokea MajiMaji FC.

"Tulianza kufanya mazungumzo na Kaheza muda mrefu kabla ya kutua Simba akitokea Majimaji hivyo kwa sasa bado yupo kwenye mipango ya timu," alieleza.

Kaheza amesema kuwa kwa sasa hana mpango wa kurejea Kenya hesabu zake ni kupata timu hapa Bongo ili kuendeleza kipaji chake.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic