July 13, 2019


MLINDA Mlango mpya wa Yanga, Metacha Mnata amesema kuwa hana hofu na changamoto mpya ambazo atazipata ndani ya kikosi chake hicho.

Mnata amejiunga na Yanga kwa kandarasi ya miaka miwili akitokea klabu ya Mbao FC.

"Najua kazi ni kubwa msimu mpya na nipo ndani ya Yanga kwa kuwa kazi yangu ni mpira, sina mashaka na kipaji changu nitapambana kufanya vema na malengo ni kuona tunabeba makombe.

"Changamoto mpya ni kitu cha kawaida kwa mchezaji hivyo ni suala la muda tu kusubiri nini kitatokea msimu ujao," amesema.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic