Huu unakuwa ni mwaka wa tano kwa tamasha hilo kufanyika mkoani Morogoro.
Mratibu wa Tamasha hilo, Mchungaji, Jerry Wyatt amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi uwanjani hapo.
"Kwa miaka minne tumekuwa na mechi kati ya Mtibwa Sugar na Mbeya City lakini mwaka huu wa tano tuna Yanga dhidi ya Mawenzi Market.
"Asubuhi ibada tutafanyia uwanjani hapo na inawezekana mchana tukawa na mechi ndogo ya kirafiki kabla ya Yanga kucheza na Mawenzi Market, tunapenda kutumia mpira kama chombo kuwajenga watu na kuwaweka pamoja na hakuna kiingilio," amesema.
Hizi sio mechi za kucheza hadhi ni ndogo mno....mnawapa fursa watani kurusha "vijembe"
ReplyDeleteSafi,watu watadharau mechi kama hizi lakini ndo zilizotusaidia kupata nafasi klabu bingwa Africa...tunaanzaga mdogomdogo then tunacheza na ma Fc Vita.
ReplyDeleteKujipima na vilabu dhaifu mwanzoni na kupata ushindi mnono wa mabao mengi utaoupa morali wachezaji ni heri kuliko kuanza na vilabu vikubwa vitavowanyima ushindi mnono kwasababu safari ndefu huanza Kwa hatua moja na kuendelea na mbili na yatatu
ReplyDeleteSiku zote unaanza na mechi rahisi ndo unakuja ngumu,so hiyo program ipo pouwaa,kabla ya Vital wacheze na mawenzi
ReplyDelete