July 9, 2019


Kocha Mkuu wa Yanga, Emmanuel Amunike amesema kuwa inawezekana Ibrahim Ajibu aliogopa kujiunga na TP Mazembe ya Congo ndiyo maana alikataa kusajiliwa.

Zahera ambaye hivi sasa anatarajiwa kutua nchini baada ya timu yake ya Taifa ya Congo kutolewa kwenye michuano ya AFCON huko Misri, ameeleza hayo kufuatia mchezaji huyo kusaini Simba.

Kocha huyo mwenye maneno mengi amefunguka kuwa hawezi kumuelezea kwa mengi Ajibu lakini akifunguka kwa kusema aliogopa kujiunga na Mazembe.

Ameongeza kwa kusema kuwa aliogopa sababu ya fedha ikielezwa kuwa dau walilotaja Mazembe lilikuwa dogo kwake.

Mbali na hilo, Zahera pia ameeleza suala la Ajibu kusaini Simba yeye kwake halina tatizo akisema kuna wachezaji wengine wengi tu ambao wanamudu nafasi yake Yanga.

Ajibu tayari ameshasaini mkataba wa miaka miwili kuichezea Simba ambayo alikuwa nayo kabla ya kwenda Yanga misimu miwili iliyopita.

6 COMMENTS:

  1. Rekebisha apo kocha wa yanga ni Mwinyi ZHera na sio Emmanuel Amunike

    ReplyDelete
  2. Bado wanamueseka Ajib walikuwa wakimuenzi na Kumuona Lulu lakini sasa wanasema alikuwa vairusi Kwa yanga

    ReplyDelete
  3. Poor journalist what longer?

    ReplyDelete
  4. umedhihirisha kuwa mnapenda sana kutunga habari.
    acheni uchonganishi

    ReplyDelete
  5. Hii habari inathibitisha ni jinsi gani mlivyo mahiri wa kutunga story.Habari imechanganywa kama kachumbari ya biriani.Shame on you guys!!!

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic