July 14, 2019


ZINEDINE Zidane meneja wa Real Madrid ameondoka katika kambi ya timu hiyo kwa dharula na kurejea nchini Canada kutokana na kupata matatizo ya kifamilia.

Meneja msaidizi David Betton kwa sasa ana jukumu la kusimamia mazoezi ya timu hiyo katika kipindi ambacho Zidane hatakuwepo.

Uongozi wa Madrid umesema kuwa kwa kipindi ambacho hatakuwepo timu itakuwa chini ya Betton.

"Kwa kipindi ambacho hatakuwepo timu itakuwa chini ya kocha msaidizi Davidd Betton,".

Zidane anatarajiwa kukaa kwenye benchi la ufundi Julai 20 ambao Madrid itacheza mchezo wa kujipima nguvu dhidi ya Bayern Munich mjini Hauston, Marekani.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic