LEO Azam FC wana kazi moja tu mbele ya Fasil Kenema ya Ethiopia kutafuta ushindi wa mapema.
Huu ni mchezo wa marudiano wa Kombe la Shirikisho baada ya ule wa awali nchini Ethiopia kupoteza kwa kufungwa bao 1-0.
Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa Azam FC, Jaffary Maganga amesema wapo tayari kwa ajili ya kutoa burudani.
"Tuko tayari kwa mapambano dhidi ya Fasil Kenema leo uwanja wetu wa machinjio, mashabiki wetu na Watanzania kiujumla tunahitaji sapoti yenu ya kutosha.
"Tuna imani ya kufanya vema na kupata matokeo chanya ni muda wa kusubiri hasa tukiwa nyumbani uwezo wa kushinda tunao," amesema.
0 COMMENTS:
Post a Comment