August 24, 2019


TIMU ya Polisi Tanzania, imetamba kuibuka na ushindi mnono dhidi ya Coastal Union katika mchezo wa ufunguzi wa Ligi Kuu Tanzania Bara utakaochezwa kesho Jumamosi kwenye Uwanja wa Ushirika uliopo Moshi mkoani Kilimanjaro.

Ofisa Habari wa Polisi Tanzania, Frank Lukwaro, alisema kikosi chao kiko vizuri kuhakikisha wanabakisha alama tatu nyumbani katika mchezo wao wa kwanza wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

“Tumejiandaa vizuri kwa mchezo dhidi ya Coastal Union, vijana wetu wako katika morali kubwa na niwaambie tu mashabiki wetu kuwa tutashinda kwa idadi kubwa ya mabao na kuongoza ligi,” alisema Lukwaro.

Katika mchezo huo, viingilio vitakuwa ni shilingi 3000 kwa mzunguko na jukwaa kuu shilingi 5000.

Polisi wanaingia kuanza mechi yao leo wakiwa na kumbukumbu ya kuifunga Yanga siku chache zilizopita mjini Moshi katika mchezo wa kirafiki kwa mabao 2-0.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic