BABA: HAKUNA STRAIKA WA KUMPITA YONDANI
BABA mzazi wa beki wa Yanga, Kelvin Yondani, mzee Patrick Yondani amefunguka kuwa kuelekea msimu mpya hana hofu na kiwango cha kijana wake huyo hata wakikutana na Simba hakuna mshambuliaji ambaye anaweza kumsumbua.
Mzee Patrick amesema kuwa Simba wao msimu huu wamesajili washambuliaji wapya lakini siyo kwamba kijana wake atashindwa kukabiliana nao.
Katika safu ya ushambuliaji, Simba imesajili wachezaji kama Deo Kanda, Wilker Henrique, Francis Kahata wakiungana na wale wa zamani ambao ni Meddie Kagere na John Bocco.
Mzee Yondani alisema kuwa beki huyo amekuwa kwenye kiwango bora kwa muda mrefu ndiyo maana amekuwa hatetereki uwanjani. Amesema ubora wa kijana wake unazidi kuimarika kadiri muda unavyozidi kwenda na pia amekuwa akizingatia yale ambayo anaelekezwa.
“Ni kweli kijana wangu Kelvin akiwa uwanjani ni mzuri na hilo wengi wanalijua, hakuna fowadi ambaye anaweza kumshinda sababu amekuwa na uwezo wa kuwasoma mapema kabla ya wao hawajamsoma na hicho ndicho kinamfanya kuwa bora.
“Hata kama wakicheza na Simba leo hii, hakuna wa kumtisha, haijalishi wamesajili mchezaji kutoka wapi, kikubwa yeye amekuwa akionyesha ubora ndiyo maana inakuwa rahisi kukabiliana na wapinzani wake.
“Nafurahia kuona kadiri muda unavyokwenda ndiyo anazidi kuitendea haki nafasi yake, nitazidi kumuombea afike mbali zaidi,” alisema mzee Yondani.








Sishangai yanayotokea Yanga kwenye mechi za kirafiki na za mashindano ya CAF nilishashauri huko nyuma kuwa Yanga inahitaji kuliimarisha benchi la Ufundi kuongeza ujuzi na mbinu kwani viwango vya wachezaji vinaporomoka kwa kiwango cha juu mno....uwezo wa benchi la ufundi la Yanga ni mdogo mno...na kama hatua za haraka hazitachukuliwa kuliimarisha benchi la ufundi kuna hatari sana huko mbele aibu itatokea...Mimi si tu kwamba ninatathmini mchezo wa soka kwa umahiri ninazichambua timu kutokana na mechi zinazocheza.....nilisema kuwa Yanga inahitaji kuiiga Simba kutafuta Kocha Msaidizi kutoka Ulaya au Hata Amerika Kusini au Asia au Hata Africa mwenye viwango vya FIFA....ili wachezaji waongezewe mbinu katika mashindano.....Bado Yanga wana wachezaji wazuri lakini soka wanalocheza watapata tabu wakicheza na timu zenye mbinu za kubadilisha mchezo haraka.....kwahiyo hili la kubadilisha au kuliimarisha benchi la ufundi haliepukiki
ReplyDeleteMimi nasema makocha waliopo yanga hawafai kabisa watawaharibia viwango wachezaji tu.
ReplyDelete