August 31, 2019


Aliyekuwa mshambuliaji wa Yanga, Mrundi, Amissi Tambwe anatarajiwa kujiunga na timu ya Fanja ya nchini Oman, Jumanne ijayo.

Tambwe ambaye kwa sasa yupo kwao Burundi atajiunga na timu hiyo baada ya kusaini mkataba wa miaka miwili ikiwa ni baada ya kufungashiwa virago na Yanga. Hata hivyo, Tambwe amelipongeza Gazeti la Championi kwa ushirikiano mkubwa alioupata katika harakati zake za kupata dili hilo.

Alisema bila ya ushirikiano huo kutoka Championi, asingefanikiwa kupata dili hilo ambalo limemwezesha kujipatia kiasi kikubwa cha fedha.

Tambwe alisema: “Natarajia kwenda kujiunga na Fanja baada ya kukamilisha kila kitu na katika timu hiyo nitamkuta Mbuyu Twite. “Nichukue nafasi hii kulipongeza Gazeti la Championi pamoja na wafanyakazi wake wote kwa ushirikiano mkubwa mliutoa kwangu mpaka nikafanikisha dili hili.

“Kuna vitu vingi ambavyo vilikuwa vikihitajika na mimi sikuwa na uwezo wa kuvipata lakini kupitia Championi nilivipata tena bila ya gharama yoyote na mwisho wa siku sasa naenda kuitumikia Fanja, hakika sina cha kuwalipa ila dua zangu nyingi nitawaombea kwa Mungu aweze kuwabariki.”

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic