August 27, 2019


DAR ES SALAAM Corridor Group, mabingwa wapya wa Kombe la Standard Chartered Bank msimu wa mwaka 2019/20 wamepata fursa ya kufanya utalii nchini England na kushuhudia mchezo wa Ligi Kuu England kati ya Liverpool na Waltford.

Akizungumza na Saleh Jembe, Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano na Masoko kutoka Standard Chartered Bank Joanith Mramba amesema kuwa wamedhamiria kuboresha mahusiano yao na wateja kwa kurejesha upendo wao kwa jamii.


"Tunafanya kazi na wateja wa aina mbalimbali nasi hatuna budi kurejesha shukrani kwao kupitia michezo na kuwapa fursa za kufanya utalii.



"Washindi wanatarajiwa kuondoka Bongo kati ya Desemba 12 ili kushuhudia mchezo kati ya Liverpool na Watford utakaopigwa uwanja wa Anfield, Desemba 14 na gharama zote zitakuwa juu yetu na watakaa kwa muda wa siku tatu, " amesema.

Mashindano hayo yalihusisha timu 28 za makampuni tofauti na msimu uliopita bingwa alikuwa ni TBL, Corridor ilishinda fainali yake mbele ya timu ya Coca-Cola kwa ushindi wa bao 1-0 lililofungwa na Iddy Clebason viwanja vya JMK Park.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic