August 27, 2019


Hamis Luwongo anayetuhumiwa kumuua na kumchoma moto mkewe, Naomi Marijani amezua kioja kingine Mahakamani Kisutu baada ya kuiomba mahakama impatie simu zake mbili, atoe pesa za kumsomesha mwanaye.

Mahakama imegoma kwa sababu simu hizo zinachunguzwa ikiwa kama sehemu ya upelelezi wa kesi yake inayomkabili.

Luwongo amerudishwa rumande na pingu miguuni kwa ajili ya kuendelea na uchunguzi wa keshi hiyo.

Hivi karibuni aliwatishiwa waandishi wa habari mahakamani hapo akidai wanampiga picha kila wakati hivyo ipo siku atakuja kuwafanyia kitu mbaya cha kuishangaza mahakama lakini Hakimu alimweleza wanahabari wapo kwenye majukumu yao na ni haki yao kumpiga picha.

Credits. Global Publishers.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic