JUZI Azam FC, ilishuhudia wapinzani wao Simba wakitwaa taji la
Ngao ya Jamii kwenye mchezo wa ufunguzi wa Ligi Kuu uliochezwa Uwanja wa Taifa
ikiwa ni mchezo wa 12 kuchezwa tangu kuazishwa michuano hiyo mwaka 2001.
Azam FC imeweka rekodi ya kibabe baada ya kushirki mashindano
hayo mara sita na kutwaa taji moja tu ambapo mwaka 2012 ilifungwa 3-2 mbele ya
Simba, 2013 ilifungwa bao 1-0 dhidi ya Yanga, 2014 ilifungwa mabao 3-0 dhidi ya
Yanga, 2015 ilifungwa kwa penalti 8-7 dhidi ya Yanga baada ya dakika 90 kutoka
sare ya bila kufungana.
Mwaka 2016 ilifanya maajabu kwa kushinda kwa penalti 4-1 mbele ya
Yanga baada ya dakika 90 kutoka sare ya kufungana mabao 2-2 na mwaka 2019
kupoteza kwa kufungwa mabao 4-2 dhidi ya Simba uwanja wa Taifa.
Ettiene Ndayiragije, Kocha Mkuu wa Azam FC amesema kuwa wameshindwa
kupata ushindi mbele ya Simba kwa kushindwa kutumia nafasi ambazo wamezipata
kwenye mchezo huo.
Yanga ndiyo walikuwa na Bahati! Simba wak vizuri sio barato hata kidogo!Azam imecheza na timu ambayo iko vizuri
ReplyDeleteAdam hawana bahati? Nafikiri!karibu Mara zote Tisa walikuwa wakicheza na favorites au more organized teams!
ReplyDelete