Mganda Jackson Mayanja, Kocha Mkuu wa KMC amesema kuwa kwa sasa kikosi chake hakijakomaa
kucheza michuano ya Kimataifa inayoandaliwa na Shirikisho la Soka Afrika (Caf) mpaka msimu ujao.
KMC
ilitolewa kwenye michuano ya Kimataifa na timu ya AS Kigali kwa kufungwa mabao
2-1 uwanja wa Taifa na imeanza ligi kwa kuchechemea baada ya kukubali kichapo
cha bao 1-0 mbele ya Azam FC.
Akizungumza
na Saleh Jembe, Mayanja amesema kuwa ametolewa mapema kutokana na kukosa
kikosi imara kwa sasa ameanza kukijenga upya kwa ajili ya ushindani.
“Michuano ya
kimataifa inahitaji wachezaji wenye uzoefu na akili jambo ambalo kwangu
lilikuwa ni tatizo kwa sasa tumeshagundua tulipokwama tunaongeza nguvu tuwe
bora zaidi
“Ushindani ndani ya ligi ni mkubwa nami
napambana kurejea kwenye ubora, wachezaji watazoea mazingira na watakuwa
wakomavu baadaye,” amesema Mayanja.
0 COMMENTS:
Post a Comment