August 27, 2019



Yule kiungo mkabaji wa Simba, Jonas Mkude leo alikosekana kwenye mazoezi ya timu hiyo yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Gymkhana, Posta jijini Dar es Salaam.


Timu hiyo inatarajiwa kucheza mchezo huo kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam kuvaana na JKT Tanzania.
Akizungumza na SalehJembe, Kocha Mkuu wa timu hiyo Mbelgiji, Patrick Aussems alisema kuwa alishindwa kufanya mazoezi hayo baada ya kupata homa.


Aussems alisema kuwa kiungo huyo atarejea uwanjani mara baada ya kupona homa hiyo aliyoipata ikiwa ni siku moja tangu waondolewe katika michuano hiyo mikubwa Afrika.


Aliongeza kuwa, tayari ameanza maandalizi ya timu hiyo kwa ajili ya mchezo wao dhidi ya JKT kwa kumuandaa mbadala wake kutokana na yeye kutokuwepo kabisa katika mchezo huo.


 “Mkude atakosekana katika mchezo wetu wa Alhamisi tutakapokuwepo uwanjani tukicheza mchezo wetu wa kwanza wa ligi baada ya kupata homa.


“Leo hakuwepo mazoezini kutokana na kuendelea na matibabu yatakayomrejesha haraka uwanjani kwa ajili michezo ijayo ya ligi,” alisema Aussems.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic