August 27, 2019


WASHINDI wawili wa Shilingi 825, 913, 640 za Jackpot Bonus ya SportPesa jana waliwasili jijini Dar es Salaam na kukabidhiwa mamilioni yao huku wakifungukia ushindi wao.

Washindi hao ni Kingsley Simon Pascal kutoka Biharamuro, Kagera na Magabe Matiku Marwa wa Mugumu, Serengeti.

Washindi hao wawili wamegawana Shilingi Mil.142 kila mmoja kati ya Mil.825 walizoshinda baada ya wote wawili kushinda ubashiri wao mechi 13 wikiendi hii.

Akizungumza na Waandishi wa Habari, Pascal ambaye ni mtumishi wa umma alisema kuwa alianza kubashiri na SportPesa tangu mwaka 2017 kabla ya wikiendi iliyopita kushinda.

Pascal alisema kuwa huo ni ushindi wake wa kwanza kuupata tangu aanze kubashiri na kushinda, hivyo anajisikia furaha.

"Leo Jumatatu ndiyo nimeanza kuamini kuwa nimeshinda rasmi licha ya kupewa taarifa na SportPesa nikiwa nyumbani Kagera.

" Niwaambie Watanzania kuwa hili jambo la ukweli kabisa na mimi ndiye mshindi halari wa jackpoti hii kubwa ya SportPesa.

"Hivyo niwatake Watanzania wote kuanza kubashiri na SportPesa ili washinde jackpot bonus mpya ya Shil Mil.200, " alisema Pascal.

Kwa upande Mama yake na mshindi huyo ambaye ni Marry Soud alisema kuwa "Nilikuwa siamini michezo hii ya kubashiri, lakini baada ya ushindi huu wa mwanangu ndiyo nimeanza kuamini.

" Mwanangu muda mrefu nilikuwa namzuia kucheza na michezo hii lakini baada ya ushindi huu nawashauri vijana wengine wacheze na SportPesa, "alisema Marry.

Kwa upande wa Marwa yeye alisema kuwa amepokea furaha kubwa ushindi wake baada ya kubashiri kwa usahihi mechi 13.

"Nianze kwa kuwashukuru SportPesa kwa kuniwezesha kubadilisha maisha baada ya ushindi nilioupata.

" Niliweka mkeka wa Shilingi 2000 ambao umeniwezesha nipate mamilioni, hivyo ninafuraha kubwa ambayo ninashindwa kuielezea.

"Hizi fedha nilizozipata nimepanga kuzifanyia mengi makubwa ni mapema kuanza kuweka wazi muda huu, acha kwanza nikakae na familia yangu baada ya hapo ntajua maana hizi fedha ni nyingi" alisema Marwa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic