August 26, 2019


Na George Mganga

Baada ya kuondolewa jana katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, Kocha Mkuu wa Simba, Patrick Aussems amekuja kivingine.

Aussems ameamua kuja na malengo ambayo kwa sasa ni kuhakikisha wanafanya vema katika mashindano yote yanayiowakabili ikiwemo taji la FA.

Kauli hiyo imekuja kutokana na Simba kuondolewa kwenye mashindano hayo makubwa na UD Songo kwa sare ya bao 1-1, mechi ikipigwa Uwanja wa Taifa.

"Malengo yetu kwa sasa ni kufanya vizuri kwenye mashindano yote kuanzia Ligi Kuu, kombe la FA na mingine ambayo tutashiriki, " amesema Aussems.

Simba imeondoshwa mashindano kutokana na faida ya bao la ugenini ambapo katika mechi ya kwanza huko Msumbiji ililazimishwa suluhu ya 0-0.

4 COMMENTS:

  1. Simba hakuna haja ya kupandisha pressure hata kidogo ni wakati wa kutulia tuli na kukiimarisha kikosi kwani timu ipo nzuri tu na kwa kiasi fulani kutolewa nje ya klabu bingwa Africa katika hatua ya awali na UD Songo wakati malengo yakiwa ni kufikia nusu fainali ni moja ya somo ya kuifanya Simba kuwa imara zaidi na nnaimani Simba itakuwa imara zaidi.
    Ila Katokana na kazia hii ya kutolewa simba mapema kunako klabu bingwa Africa kuna mambo ya dhahiri yamechangia na hakuna haja ya kumtafuta mchawi. Kwa maoni yangu bila ya kumumunya maneno.
    Tatizo la kwanza ni ...
    (1) kocha wa Simba. Tabia ya kocha wa Simba ya kuwa na mfumo mmoja tu wa kutafuta ushindi ni tatizo. Mfano mwaka jana Simba ilifanikiwa kufika mbali klabu bingwa Africa kwa kusubiri ushindi kwenye uwanja wake wa nyumbani. Mbinu hiyo kwa namna yeyote wapinzani wa Simba waliishajua na ilikuwa rahisi na kwa timu pinzani kupindua meza ndani ya Dar. Kocha wa Simba alitakiwa kubadilika kwenye mechi za ugenini tangu mwaka jana lakini akashindwa kufanaya hivyo na kama haitoshi akarejea tana klabu bingwa Africa na hali ya kusua kusua katika mechi za ugenini na kama UD Songo wangekuwa makini kule Msumbiji basi wangeifunga Simba si chini ya goli nne. Na kwa kiwango kile dhaifu cha mchezo walichokionesha Simba ugenini zidi ya UD Songo ndicho kilichowapa nguvu UD Songo ya kuaamini yakuwa hakuna shaka yeyote wanauwezo wa kuwaondosha Simba.Kimsingi UD Songo waliifunga Simba tangu mechi ya mwanzo na walikuja tanzania kumaliza kazi tu.
    (2) sababu ya pili ya Simba kutupwa nje ya klabu bingwa Africa ni Kocha vile vile.Kitendo cha kocha wa Simba kushindwa kurekebisha tatizo la beki yake lililodumu zaidi ya mwaka sasa ndio liloigharimu Simba tena kukubali bao la mapema na ndilo lilowaondoa mashindano.
    (3) sababu ya tatu ya Simba kutupwa nje ya klabu bingwa Africa ni kocha wao vile vile. Kitendo cha kocha wa Simba kung'ang'ania baadhi ya wachezaji fulani licha ya kufanya makosa ya wazi ya kujirejea mara kwa mara imechangia Simba kutupwa nje. Niliwahi kuandika waraka juu ya madhaifu ya beki ya Simba na jinsi kocha wa Simba anavyoshindwa kulitatua tatizo hilo licha ya Simba yakuwa na rundo la mabeki.Na si kama mabeki hakuna Simba hapana ila kocha mwenyewe ana mabeki wake ndio hao hao hata wakicheza hovyo. Kocha wa Simba si kocha mwenye kujiamini na mara nyingi huwaondelea hali ya kujiamini wachezaji wake vile vile pia. Kwa mfano mechi ya juzi nnaimani kubwa kama Mlipili na Kennedy wangepewa nafasi wasingefanya makosa ya yale tuliyoyaona yakifanywa na beki ya Simba na kusababisha goli. Nnaimani kabisa samata angekuwa chini ya Aussems sidhani kama angetoboa. Patric phiri alikuwa na ujasri wa kwaamini wachezaji wake hasa wale wale wadogo.kwanza kwanini kocha alimuondoa kakolanya golini akiwa yupo kwenye fomu?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Very professional analysis...
      Simba tatizo kubwa ni mbinu na woga wa mwalimu....Ausems ananaamini ktk experience na sio efficiency....Mkude+Wawa licha ya kuwa na viwango duni lkn anawachrzesha...Manula toka arudi kujiunga na stars amekuja ku train na wenzie siku 3 kabla kisha anamweka Beno ambaye amecheza friendly match zote+simba day.Ikumbukwe malengo ya simba ni kuwa mabingwa wa CL ndani ya miaka 5 ijayo lkn Ausems alikataa kusaini mkataba wa miaka miwili.Simba ina kikosi kizuri na kikipata kocha anajua kuwatumia wachezaji tutachukua ndoo na kufika mbali CL hapo mwakani.Ausems ameshindwa kuinua vipaji vya wachezaji wachanga...hadi mechi ya kirafiki anatumia wakongwe...kitu hambacho kitafanya kila msimu club ihanhaike kutafuta wazoefu

      Delete
    2. Hio namba tatu napenda niongeze, kocha ana imani na wawa, nyoni, mkude, chama n ao watu unaweza kuona wakicheza wana makosa mengi na pia wapozesha sana mpira kwa kuwa hawana kasi na maamuzi ya haraka, juzi mkude na wawa walipoteza mipira maeneo hatari, lile kosa la Wawa likazaa faulu ambayo ilizaa goli lakini kabla ya hapo Mkude na Nyoni walisha sababisha timu ikoswe koswe kufungwa. Chama yko slow na maamuzi ya kutoa pasi au kupiga mashuti golini ni finyu sanaaa... Namkumbuka Okwi na Kichuya hawa watu walikuwa wanakaba kila wakipoteza mpira wakati Chama hakabi hata akipoteza mpira.. mimi imani yangu inaniambia ukabaji huanzia kwa washambuliaji then mabeki na viungo wakabaji wanamaliza kazi.. wale UD songo walikuwa wakaba mpaka kipa wetu, nafikiri unakumbuka kosa alilo taka kufanya Manula wakati akishindwa kupiga mpira mbele kwa wakati na kidgo tu afungwe... Patrick inabidi awe mkali kwa wachezaji na pia awafundishe mbinu nyingine za ukabaji na ushambulijaji... Hili ni gonjwa sugu na kama hatalirekebisha hakuna matokeo mazuri msimu huu kwani timu zimejiandaa na mdhamini yupo...

      Delete
    3. Sio awe mkali tu bali aondoe u father kwenye timu....wachezaji wote wapewe nafasi sawa ya kupambania namba.....sio kuna watu anawapanga licha ya kila cku kuwa na makosa yaleyale

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic