August 28, 2019


INAELEZWA kuwa kocha wa Yanga, Mwinyi Zahera ameanza kupata wakati mgumu juu ya nani awe kipa namba moja kutokana na kiwango cha juu anachokionyeha Metacha Mnata.

Zahera alimsajili Metacha kuwa kipa namba mbili nyuma ya Mkenya Farouk Shikalo lakini hali imeanza kubadilika baada ya Shikalo kuzikosa mechi mbili za Ligi ya Mabingwa Afrika kwa kukosa leseni ya kushiriki michuano hiyo na nafasi yake kuchukuliwa na Metacha.

Metacha alikuwa shujaa wa mchezo akiisaidia Yanga kuondoka na ushindi muhimu wa bao 1-0 ugenini dhidi ya Township Rollers na kufanikiwa kusonga mbele kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kudaka mkwaju wa penalti na kuokoa hatari nyingi katika lango lake.

Chanzo cha kuaminika kutoka ndani Yanga kililiambia Championi Jumatatu kuwa kwa sasa Zahera anapata wakati mgumu kwa kiwango anachoendelea kuonyesha Metacha, hajui nani awe namba mbili kati yake na Shikalo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic