MSEMAJI MPYA YANGA APATIKANA
Tunaweza kusema kuwa kile kilio cha mashabiki na wanachama wengi wa Yanga kutaka Dismas Ten aondolewe katika nafasi ya usemaji na badala yake atafutwe mtu mwingine inaweza kuwa imepatikana.
Taarifa zinasema kuwa mwanachama na shabiki wa Yanga, Antonio Nugaz, ambaye pia ni mtangazaji katika kituo cha Clouds Media Group, anatajwa kuchukua nafasi ya Dismas Ten.
Nugaz ambaye amekuwa akijitahidi kuhudhuria mechi nyingi za Yanga, leo ameonekana akiwa na Dismas Ten ambaye alikuwa kwenye nafasi hiyo.
Taarifa zilizo ndani ya Yanga zinasema kuwa Nugaz anaweza akatangazwa muda wowote kuanzia sasa kurithi nafasi hiyo iliyopooza kama mashabiki wengi wa Yanga wanavyosema.
Hatomuweza Haji Manara
ReplyDeleteUfundishaji wa Zahera lazima ubadilike ama kuimprove haswa kufanya timu icheze soka la Ushirikiano na pia pasi zenye malengo na ukabaji wa pamoja. Halafu kusiwe na papara ya kuharakisha kufika mbele ili kufunga bila ya kuwa na mipango mtaendaje kama timu mkiwa mnashambulia na mkiwa mnarudi...viungo wa ushambuliaji, mawingi na wafungaji wa mbele wawe na mawasiliano watoe uchoyo wawe na utulivu kuanzia mita 20 na kuendelea wanapofika lango la adui wawe na akili namna ya kuipenya ngome ya timu upinzani....haya ndiyo makosa ya kiufundi
ReplyDeleteMFIKISHIENI MWINYI ZAHERA
Zahera amekuwa mwingi wa kujitetea na kuwaangushia lawama wengine, naungana na wewe time is running out muda si mrefu uvumilivu utafika mwisho.
DeleteU20 Cecafa inaingiliana na mashindano ya CAF CL na Ligi Kuu.....sasa sijui ni kwa mantiki ipi TFF inatangaza majina ya wachezaji 35 kuunda timu katika majina hayo wanajumiuishwa wachezaji wa Azam (Oscar Maasai na wengine) na Yanga (Kabwili na Gustafa) ambao wapo kwenye maandalizi ya mechi za mashindano ya CAF??? Haya mashindano u20 cecafa yapo kwenye ratiba ya vilabu walijulishwa mapema??? Haya ni maswali ambayo hayana majibu bado!
ReplyDeleteSoka letu ni sukuma tuende,hakuna malengo muhimu
ReplyDeleteHatuhitaji mropokaji kama manara....anatakiwa msemaji/afisa habar mwenye weledi
ReplyDelete