JUMA Kaseja, nahodha msaidizi wa timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' amesema kuwa siri kubwa ya ushindi ni kujiamini na kufanya kazi kwa kushirikiana.
Jana Stars ilishinda mchezo wake wa marudiano dhidi ya Kenya kwa penalti 5-1 kwenye mchezo wa kutafuta tiketi ya kufuzu michuano ya Chan inayotarajiwa kufanyika Cameroon 2020.
"Tunafanya kazi kwa ajili ya Taifa na kila mmoja anajua kwamba kikubwa ambacho mashabiki na watanzania wanakihitaji ni kupata ushindi kwenye michezo ambayo tunacheza hivyo ushindi wetu ni zawadi kwa watanzania na mashabiki wetu kiujumla," amesema.
Hatua inayofuata kwa Stars ni mchezo dhidi ya Sudan kabla ya kufuz michuano ya Chan.
Safi kabisa ila benchi la ufundi waanze kuwaandaa na kuwaamini ushambuliaji chipukizi kuliko kujiridhisha na washambuliaji wakongwe peke yake. Kuwepo na mikakati maalum ya kuwawezesha washambuliaji chipukizi kwani kukosekana kwa akina Samata ndani ya taifa stars kwenye chan ambao hawawezi kutumika kwenye mashindano haya kumekuwepo na tatizo kubwa la utupiaji magoli ndani ya Taifa stars.Na wachezaji nao hasa vijana haya mashindano ya Chan ni vita yao. Ni nafasi adimu ya kuonesha uwezo wao.Ni nafasi ya kutengeneza Taifa stars mpya itakayowaletea raha watanzania. Kwenye nia pana njia na kunako jitihada ndio njia pekee ya kutafuta msaada na kama hautatoka kwa mwanadamu basi Mungu kamwe hamuachi mkono mwenye kujitahidi kwa dhati. Tunawaomba tu benchi la ufundi wasichoke kutafuta wachezaji wenye uwezo hasa vijana na kuwajumuisha kwenye program yao ya kuijenga Taifa stars imara. Tunaimani sana na benchi hili la ufundi katika kuiendeleza timu ya Taifa na Mungu atawasaidia Ameni .
ReplyDelete