August 28, 2019


Baada ya Simba kutolewa katika michuano ya kimataifa, kiungo wa timu hiyo, Said Ndemla amesema kuwa inahitajika juhudi kubwa kwa sasa kupata nafasi ya kucheza katika kikosi hicho.

Mchezaji huyo awali alikuwa akitegemea kupata nafasi katika kikosi cha kwanza endapo wachezaji wengine watakuwa wameiwakilisha Simba katika michuano ya kimataifa, jambo ambalo kwa sasa halipo kutokana Simba kutolewa.

Ndemla alisema kuwa Simba ina wachezaji wengi sana haswa katika eneo la kiungo, msimu uliopita alipata nafasi baada ya wachezaji wengine kupumzishwa kutokana na kucheza mechi za kimataifa, hivyo baada ya Simba kutolewa mapema itabidi ajitume zaidi ili apate nafasi ya kucheza.

“Simba kuna wachezaji wengi kwenye eneo la kiungo, msimu uliopita nilipata nafasi ya kuanza kwenye mechi ya ligi kutokana na wachezaji wengine kutoka kwenye mechi za kimataifa, msimu huu tumetoka mapema hivyo hakuna jinsi itabidi nipambane ili nimshawishi kocha anipe nafasi,” alisema Ndemla.

2 COMMENTS:

  1. Tafuta timu nje ucheze au mpira wako utaishia hapa wakati bado unachokipaji

    ReplyDelete
    Replies
    1. nje na huku alishaenda majaribio kibao, ndg vp?, yeye angefanya maamuzi magumu aende timu atakayopata namba ya kudumu, lakini pia kwa simba pale namba ni ngumu kwa demla.

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic