MCHEZO wa watani wa jadi wa Madrid, Atletico Madrid na Real Madrid unatazamiwa kuchezwa Septemba 28 Uwanja wa Wanda Metropolitan.
Atletico Madrid watakuwa wenyeji wa mchezo huo wa kibabe unaosubiriwa kwa shauku kubwa na mashabiki.
Pambano hilo la miamba ya Madrid ambalo limepewa jina la 'El Derbi Madrileno' linatarajiwa kusisimua kutokana na mipango ya timu zote kutaka kutwaa ubingwa wa La Liga.
Timu hizi zinapewa nafasi ya kutoa upinzani wa kutisha Kwa Barcelona ambao ni Mabingwa watetezi.
Real Madrid alinyooshwa kwa mabao 7-3 kwenye mechi ya kujipima hivi karibuni nchini Marekani hivyo Meneja, Zinedine Zidane ana kazi ya kufanya kufuta aibu hiyo.
0 COMMENTS:
Post a Comment