August 5, 2019


DIANA Msemwa, mchezaji wa timu ya Taifa ya Tanzania ya Wanawake chini ya miaka 20 'Tanzanite' ameweka rekodi ya kutwaa tuzo mara mbili kwenye mechi za michuano ya COSAFA.

Michuano hiyo inayoendelea nchini Afrika Kusini, Tanzanite imeitwa kushiriki michuano hiyo ya kimataifa.

Msemwa alitwaa tuzo ya mchezaji bora kwenye mchezo wa kwanza dhidi ya Botswana ambapo Tanzanite ilishinda mabao 2-0 kisha jana alitwaa tuzo hiyo wakati Tanzanite ikiibuka na ushindi wa mabao 8-0.

Mechi zote mbili zimechezwa uwanja wa Gelvalander, Port Elizabeth nhini Afrika Kusini.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic