August 4, 2019


CHRISTOPHER Galtier, Meneja wa Lille amesema kuwa ameshangazwa na kitendo cha nyota wa kikosi hicho Nicolas Pepe kujiunga na Arsenal.

Meneja huyo amesema kuwa Arsenal haikuwa chaguo la kwanza kwa nyota huyo na anasikitika kwa kuwa hatacheza Ligi ya Mabingwa.

Nyota huyo anayekipiga timu ya Taifa ya Ivory Coast amekamilisha dili lake kwa dau la pauni milioni 72 na ametua ndani ya Arsenal baada ya kupigana vikumbo na Napol pamoja na Bayern Munich ambao walikuwa wanaiwinda saini yake.

Galtier anaamini Bayern Munich ilikuwa sehemu sahihi Kwa Pepe kuliko Arsenal ambapo yupo huku akimpigia hesabu ni namna gani anaweza kuwa winga bora ndani ya Premier League. 


"Sehemu sahihi kwake nadhani labda Bayern Munich Kwa kuwa pale angepata nafasi ya kucheza pia nawatambua vizuri, (Frank) Ribery na (Arjen) Robben wanaondoka," amesema.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic