BAKARI Malima 'Jembe Ulaya' ambaye ni nyota wa zamani wa timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' leo amezungumza na wachezaji wa kikosi hicho muda mchache kabla ya kuwavaa Kenya.
Stars leo ina kibarua cha kutafuta ushindi ugenini kwa ajili kukata tiketi ya kufuzu michuano ya Chan baada ya mchezo wa kwanza kutoshana nguvu bila kufungana uwanja wa Taifa.
Malima amesema kuwa amewajenga kisaikolojia wachezaji na kuwaambia kwamba wanaweza kupata matokeo chanya.
"Nimewaambia ukweli kwamba wana kazi ngumu ya kufanya ila wanaweza kwa kuwa uwezo wanao pia michezo ya ushindani hasa ukiwa ugenini mara nyingi presha huwa inakuwa kwa mwenyeji.
"Hivyo nimewaambia kwamba wasiwe na presha wacheze kwa kujiamini kwani inawezekana kwao kupata matokeo chanya," amesema.
0 COMMENTS:
Post a Comment