WACHEZAJI wa Simba leo watapiga picha na mashabiki wao ambao wamenunua tikite za Platinum Plus pamoja na zile za Platinum katika hotel ya Serena.
Zoezi hili ni malumu kwa ajili ya kuelekea SportPesa Simba wiki inayotarajiwa kufika kilele Agosti 6 uwanja wa Taifa.
Siku hiyo ya kilele Simba itacheza mchezo wa kirafiki na timu ya Power Dynamo pia itakuwa siku rasmi kwa Simba kutambulisha jezi mpya pamoja na wachezaji wake wote.
Pia leo Simba itatembelea kituo cha watoto yatima cha Kurasini kwa lengo la kuwaona na kutoa misaada kwa watoto hao.
0 COMMENTS:
Post a Comment