STARS: TUPO TAYARI KUIMALIZA BURUNDI
Kocha msaidizi wa Taifa Stars, Seleman Matola amesema kuwa ana imani kikosi kitakwenda kufanya kweli kwenye mchezo wao wa kufuzu Kombe la Dunia dhidi ya Burundi.
Stars itamenyana na Burundi Jumatano hii kwenye Uwanja wa Prince Louis Rwagasore nchini Burundi kabla ya kurudiana nao uwanja wa Taifa, Septemba 8 mwaka huu.
Matola undi alisema kuwa wachezaji wana morali kubwa ya kupambana na kila mmoja anatimiza jukumu lake kwa wakati.
“Tuna kazi ngumu ya kufanya hasa ukizingatia tutakuwa ugenini jambo ambalo limetufanya tutumie muda mwingi kuwaandaa wachezaji wetu.
“Matumaini ya kufanya vizuri ni makubwa kikubwa ni sapoti ya mashabiki kuelekea kwenye mchezo wetu kwani hesabu zetu ni kupata matokeo mazuri,” alisema Matola ambaye ni Kocha wa Polisi Tanzania ya Kilimanjaro.
0 COMMENTS:
Post a Comment