TOWNSHIP ROLLERS!!! MBONA WANAKAA MAPEMA TU, MSOME ZAHERA ANACHOKISEMA
Achana na presha waliyokuwa nayo wapinzani wao, Township Rollers ya Botswana, unaambiwa Kocha Mkuu wa Yanga Mkongomani, Mwinyi Zahera amepanga kumaliza shoo ndani ya dakika 10 za mwanzo za mchezo.
Mabosi wa Rollers hivi sasa wanahaha kuhakikisha wanawaondoa Yanga kwa kutumia njia ya hujuma ikiwemo iliyokataliwa na Shirikisho la Soka Afrika (Caf) ambalo liliandikiwa barua ya kubadili uwanja kabla ya kukataliwa ombi lao.
Hivyo, washambuliaji wa Yanga wakiongozwa na Juma Balinya, Patrick Sibomana, Sadney Urikhob wana kibarua kigumu cha kuhakikisha wanafanyia kazi maelekezo ya kocha wao.
Zahera alisema kuwa kikubwa anataka kuona timu yake inapata bao la mapema na ndani ya dakika 10 za mwanzo wawe wanaongoza.
Zahera alisema kuwa katika mchezo uliopita uliopigwa Uwanja wa Taifa jijini Dar, wachezaji walishindwa kucheza kwa kufuata maelekezo yake na kusababisha watoke sare hiyo ambayo ni mbaya kwao.
“Katika mchezo huu ninataka tucheze kwa malengo, kwani ni lazima tushinde kama kweli tunataka kusonga mbele kwenye mashindano haya makubwa Afrika na hilo linawezekana kwetu kutokana na maandalizi niliyoyafanya.
“Kama tuliweza kufunga bao tukiwa nyumbani kwa nini tushindwe kufunga hapa ugenini, kikubwa kinachotakiwa ni kucheza kwa tahadhari ya kuwahofia wapinzani wetu ambao nao wapo vizuri,” alisema Zahera.








Wakati Yanga na kocha wao wanapanga kuzitumia dakika 10 za mwanzo kupata bao ugenini lakini pia Yanga wanatakiwa kuwa makini sana kupita maelezo katika dakika 20 za mwanzo wa mchezo na kama ningekuwa Zahera basi nisingekimbilia kutafuta goli la mapema ugenini na badala yake ningewapanga wachezaji wangu kujilinda zaidi dakika za mwanzo na kuwasoma kwa haraka mbinu zao ili kujua ubora wao upo wapi na kufanya mashambuzi ya kushtukiza. Yanga sio vibaya kama watawaangalia As Kigali jinsi walivyocheza ugenini zidi ya KMC.
ReplyDeleteUmesema vizuri...kushambulia mno bila kuweka tahadhari ya kujilinda nyuma ni hatari kwa Yanga lazima ulinzi uimarishwe sambamba na kushambulia mfululizo
DeleteDon't sail out further than you can row back.
ReplyDeleteTownship rollers waliifunga Dar mapema tu!Kilichofuatia ni nini? Mbona Yanga hakutumia hii strategy alipocheza na Polisi....AFC leopard wenyewe walifungwa usiku wa manane!
ReplyDelete