ZAHERA AANZA NYODO YANGA
Wakati huohuo, Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera ameahidi kuwa na msimu mzuri huku akitamba kuchukua kila kombe watakalolishindania likiwemo la Ligi Kuu Bara.
Ametoa kauli hiyo wakati wakiwa kwenye Chuo cha Mwika Wildlife maeneo ya Moshi mkoani Kilimanjaro ambako wameweka kambi kujiandaa na mchezo wa marudiano wa Raundi ya Awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Township Rollers ya Botswana.
“Nimefanya maboresho makubwa ya kikosi changu hali inayonipa matumaini ya kuchukua kila ubingwa tutakaoushindania katika msimu huu na hilo linawezekana kwangu.
“Nataka msimu huu kuchukua ubingwa wa ligi na Kombe la FA mfululizo na kufika mbali katika Ligi ya Mabingwa Afrika, tutaanza kwa kuwaondoa Township ili tusonge mbele zaidi,” alisema Zahera.
Ikumbukwe kuwa, msimu uliopita Yanga ilimaliza ligi kuu ikiwa nafasi ya pili nyuma ya Simba iliyotwaa ubingwa, pia iliishia Hatua ya Nusu Fainali ya Kombe la FA.








Ni vyema kuwa na matumaini ya kufanya vizuri lakini inapashwa kujiandaa vyema kutokeza hicho unachotaka kitokee. Ni bore kuwa na wachezaji wachache wanaojituma kuleta matokeo badala ya kuwa na wachezaji wengi ambao hawawezi kuleta matokeo. Matokeo ya mchezo wa jana hayaonyeshi yasemwayo hivyo tunapashwa kujitathmini sasa.
ReplyDeleteZahera asiongee lolote kwani kikosi kina ubora ila benchi la ufundi halina ubora.
ReplyDeleteSishangai yanayotokea Yanga kwenye mechi za kirafiki na za mashindano ya CAF nilishashauri huko nyuma kuwa Yanga inahitaji kuliimarisha benchi la Ufundi kuongeza ujuzi na mbinu kwani viwango vya wachezaji vinaporomoka kwa kiwango cha juu mno....uwezo wa benchi la ufundi la Yanga ni mdogo mno...na kama hatua za haraka hazitachukuliwa kuliimarisha benchi la ufundi kuna hatari sana huko mbele aibu itatokea...Mimi si tu kwamba ninatathmini mchezo wa soka kwa umahiri ninazichambua timu kutokana na mechi zinazocheza.....nilisema kuwa Yanga inahitaji kuiiga Simba kutafuta Kocha Msaidizi kutoka Ulaya au Hata Amerika Kusini au Asia au Hata Africa mwenye viwango vya FIFA....ili wachezaji waongezewe mbinu katika mashindano.....Bado Yanga wana wachezaji wazuri lakini soka wanalocheza watapata tabu wakicheza na timu zenye mbinu za kubadilisha mchezo haraka.....kwahiyo hili la kubadilisha au kuliimarisha benchi la ufundi haliepukiki
ReplyDelete