KOCHA Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera amesema kuwa bado kikosi chake hakijawa na maelewano mazuri jambo ambalo liliwapa taabu kupata matokeo kwenye mchezo wao wa kwanza dhidi ya Township Rollers.
Yanga jana imelazimisha sare dhidi ya Township Rollers, mchezo uliochezwa uwanja wa Taifa kwa kufungana bao 1-1.
Mchezo wa marudiano wa kimataifa unatarajiwa kuchezwa kati ya Agosti 23-25 nchini Botswana.
"Wachezaji wangu bado wanasumbuliwa na tatizo la kushindwa kuelewana wakiwa ndani ya uwanja jambo ambalo linaleta ugumu kwenye kupata matokeo uwanjani.
"Kwa sasa hesabu ni kuona kwamba tunakuwa na kikosi imara ambacho kitapata matokeo kwenye mchezo wetu wa marudio, mashabiki waendelee kutupa sapoti katika hili, nami nitafanyia kazi makosa yote," amesema.
Vipi utawapata mashabiki nanyi mpo ugenini iliobaki nikuomba miujiza Mungu ateremshe msaada
ReplyDeleteHuenda mlilolikosa nyumbani mkalipata ugenini
ReplyDeleteSio rahisi kukipata ugenini ulichokipoteza nyumbani..Mfani ni mechi ya Swaziland tu ndiyo Simba mwaka jana ilifanikisha ugenini.. Zingine zote walikuwa wanapigwa kuzanzia 3 na mara mbili mfululizo 5-0
DeleteMechi 1 walifungwa 2-0 na mechi moja 2-1.Mechi za Ligi hazijalishi unafungwa ngapi au unafunga ngapi?Mwisho ni pointi 3.
ReplyDeleteKwenye mtoano away goal ni advantage kwa timu iliyochezwa ugenini.
Ligi ya mabingwa Africa imekuja mapema ni kama imezikuta timu nyingi kama vile mtu anaetoka kuamka asubuhi hasa kwa timu kama Yanga ambayo hatukujua wataanzia ghafla kama tungepata nafasi za nyongeza za ushiriki mwaka huu. Tatizo kubwa la Yanga kama timu nyingi ni wale wachezaji wapya kukosa muunganiko ndani ya timu na ndio maana utaona ujanja alioutumia kocha wa Simba kwenye mechi na wamakonde alianza wachezaji watatu tu wageni kwenye kikosi cha
ReplyDeletekilichoanza Msumbiji kati ya wachezaji wapya kumi au kumi Na 12 waliosajiliwa ndani ya simba.Na hapa ndipo Yanga walipokosea kwenye mechi na Waswana kwani wangeanza na Yondani,Dante,Juma Abduli hata haji mwinyi kushoto na ngasa,kaseke hawa wachezaji wagepeleka muunganiko mzuri mbele na nyongeza ya wachezaji wageni basi isingezidi wachezaji watatu. Siri kubwa ya timu kufanya vizuri sio mkusanyiko wa wachezaji wazuri bali ni mkusanyiko wa maelewano baina ya wachezaji waliokaa pamoja kwa muda mrefu pamoja na ubora wa benchi lao la ufundi.
Si Ni Yanga hii hii iliyokuwa inafunga 10, 7, 4...huo si muunganiko tosha!!! Labda kama walicheza na timu ambazo hazikuwa na uwezo!
ReplyDeleteYanga ina nafasi kubwa ya kuibuka mshindi mechi ijayo,kwa sababu wafungaji wana ari ya kupata magoli
ReplyDelete