ZAHERA ATAJA IDADI YA SUTI ANAZOMILIKI
Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera amesema kuwa ana suti zaidi ya pea 100 kabatini ambazo ataanza kutupia kila anapokuwa kwenye benchi la ufundi wakati wa mechi.
Kutokana na kanuni zilizotolewa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kupitia Bodi ya Ligi ni kwamba msimu huu watu wote wa kwenye benchi la ufundi ni lazima wavae sare na mavazi ya heshima, atakayekiuka adhabu inamhusu.
Zahera ambaye mchezo wake wa kwanza wa ligi alipoteza mbele ya Ruvu Shooting kwa kufungwa bao 1-0 ambapo alivaa ‘pensi’ kama kawaida yake alisema hakuwa na taarifa hizo.
“Sikuwa na taarifa kuhusu kuvaa sare na ninazipata taarifa muda huu, ila kama wanahitaji niwe navaa suti hilo siyo tatizo nina masuti mengi kabatini zaidi ya mia nitaanza kuzivaa kuanzia mechi zinazofuata,” alisema Zahera
Basi hizo suti Mia ndizo zitazoipa Yanga ubingwa Kwa msimu huu na kusonga mbele katika mechi nyingi za shirikisho. Tusubiri safari ndio imeanza Kwa gia ya kwanza tu tungoje yapili na yatatu mambo yatanona
ReplyDelete