MEDDIE Kagere, mshambuliaji wa Simba ametangazwa na Kamati ya Tuzo ya Ligi Kuu Bara kuwa
mchezaji Bora wa mwezi Agosti.
Kagere
amepewa tuzo hiyo akiwashinda wachezaji wenzake ambao alifika nao fainali ambao
ni Lukas Kikoti wa Namungo na Seif Karihe wa Lipuli.
Kagere msimu
huu ametimiza majukumu yake mbele ya wapinzani wake JKT Tanzania kwenye mchezo
wa kwanza uliochezwa uwanja wa Taifa kwa kuifanya timu yake kutwaa pointi tatu muhimu kwenye ushindi wa mabao 3-1 yeye alifunga mawili na kutoa pasi moja ya bao lililofungwa na Miraj Athuman uwanja wa Uhuru.
0 COMMENTS:
Post a Comment