September 6, 2019


JOSE Mourinho aliyekuwa meneja wa Manchester United inaelezwa kuwa alimchunia jumla beki wa Liverpool, Virgil Van Dijk.

United ilikuwa kwenye harakati za kuinasa saini ya beki huyo ambaye ana tuzo ya Beki Bora wa Ulaya kwa sasa pia anawania Tuzo ya Ballon d'Or akiwa ametimiza jukumu la kuipa timu yake taji la ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu uliopita.

Taarifa zinadai kuwa Mourinho aliwaambia mabosi wake kuwa hesabu zake kubwa ni kwa Eric Bailly na Victor Lindelof ambao alikuwa anawaamini. 

Baada ya msimu mmoja kumkataa beki huyo raia wa Uholanzi Mourinho alifukuzwa kazi msimu wa mwaka 2018 kutokana na matokeo mabovu na hatimaye United imetoa paauni milioni 85 kumpata beki wa kati Harry Maguire kiwango ambacho ni kikubwa kinoma.

2 COMMENTS:

  1. Uongo mtupu. Kiingereza kinawasumbua, hapo ndo ilibaki kidogo?

    ReplyDelete
  2. Hahahah nmesom kuutafuta huo ukarb kidg cjauona

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic