BRUNO Tarimo ‘Vifuaviwili’ bondia wa ngumi za kulipwa ambaye
ni bingwa wa International Super Feather
Weight ambao ameupaata hivi karibuni nchini Serbia kwa kumtwanga kwa pointi
bondia Scheka Gurdijeljac raia wa Serbia amesema kuwa ishu inayompasua kichwa
ni lugha tu.
Vifuaviwili amesema kuwa
kila anaposkia kuna pambanao mbele yake nje ya nchi hata ndani hana mashaka ya
kupata ushindi kinachompa ugumu ni mawasiliano hasa wa lugha za kigeni kutokana
na kutokuwa na elimu ya kutosha.
“Unajua elimu yangu mimi darasa la saba sasa ninapokuwa na
kazi nje wao hawajui Kiswahili kabisa wala kiingereza ambacho ninakijua mimi
kuna wengine hawajui hapo ndio tatizo lilipojificha na huwa ninapata taabu
kidogo.
“Ila kikubwa ambacho kinanifanya nielewe huwa ninakuwa na
mtu ambaye ni mtaalamu wa lugha yeye ananisaidia kuelewa na nikikaa sehemu kwa
muda kidogo huwa naweza kujibadili kutokana na mazingira ili kuelewa kinachozungumzwa,”
amesema Vifuaviwili.
0 COMMENTS:
Post a Comment