HUJUMA ZA ZESCO, YANGA WAKATIWA UMEME NDOLA
Unaweza kusema ni kama hujuma maana tangu mabosi Yanga watue katika mji wa Ndola, Zambia wamekuwa wakikatiwa umeme mara kwa mara, jambo ambalo limesababisha mawasiliano kuwa magumu.
Mabosi hao wapo Ndola tangu Jumapili iliyopita kwa ajili kufanya maandalizi ya mechi dhidi ya Zesco ambayo ni ya raundi ya pili ya ligi ya Mabingwa Afrika itakayofanyika leo kwenye uwanja wa Levy Mwanawasa.
Mbali na umeme pia kumeuwa na shida ya mtandao ambao umesababisha kusiwe na mawasiliano mazuri baina yao kama viongozi na hata wachezaji.
Kaimu Mwenyekiti wa Yanga amekiri uwepo wa tatizo hilo kuwa limesababisha changamoto kwao kama viongozi.
"Tangu tumefika hapa kumekuwa hakuna huduma nzuri ya umeme maeneo mengi, hata hotelini tulipofikia kwani unapatikana kwa saa chache na ndiyo sababu unaona muda mwingine sipo hewani", alisema Msolla.








Subirini mchezo uchezwe jamani msijipe matumaini wakati hata mchezo haujachezwa mwishowe mtakuja kulia na kuumia....hili ni tatizo kubwa la timu matokeo ya soka wanakuwa nayo mdomoni na propaganda kibao halafu mwisho wa siku matokeo yanakuwa tofauti hapo ndipo unaposikia watu wamekufa wengine wako mahututi wengine wamezimia subirini dakika 90+ ziishe na matokeo yatajulikana....kwasasa hivi muwe wakimya kwani hamjui au hakuna mtu anayejua matokeo mpaka dk 90 za mchezo!
ReplyDeleteUmeme kote duniani na hapa kwetu kila kukicha unakatika. Leo Zambia kukatika Umeme imekuwa wamekusudiwa Yanga. Hii si nzuri. It is funny and strange
ReplyDeleteUsiseme kote duniani..sijui kama unajua mfumo wa kwetu huku kuhusu umeme??umeme haukatiki ukikataika mnakuwa na taarifa. Hii Zesco ni mali ya TANESCO ya hapa Zambia (ZESCO) kila kitu kinawezekana
Deletekwani huwajui watz kunifanya wanajua kila kitu,
Deleteyaani ushabiki wetu huku bongo ninsawa na uadui.
mwingine anasema tusijipe moyo tusubir matokeo, hiyo nayo inahitaji kupima kweli.
figisu zipo sana tu, hata simba walilalamika sana hadi waliandikia fifa barua dhidi ya kutolewa mwamuz wa awali dhidi ya mechi yao na Tp mazembe, leo wao wanaona hii si figisu kwa holtel kubwa kukosa njia mbadala ya umeme