September 15, 2019


IMERIPOTIWA kuwa dili la Paul Pogba, kiungo mshambuliaji juu ya kusepa ndani ya Manchester United lilikuwa limetiki na alikubali kulipwa mshahara wa pauni 429,000 (bilioni 1.2) ndani ya PSG.

Inadaiwa kuwa dili hilo lilikuwa mwishoni kutiki ila liliyeyuka na kubuma baada ya Neymar Jr kufeli kujiunga na Barcelona.

Kiungo huyo raia wa Ufaransa alikuwa mbioni kusepa Old Trafford baada ya kuhusishwa na Barcelona, Real Madrid na PSG wakati wa dirisha la usajili uliopita.

Chombo kimoja cha habari nchini Italia kimeeleza kuwa dili hilo lilifika pazuri na United walikuwa tayari kumuuza Pogba kama PSG wangetimiza kile walichokubaliana.



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic