September 15, 2019


REAL Madrid iliyo chini ya Meneja Zinedine Zidane inaelezwa kuwa bado inaendelea kujijenga na sasa imewaibukia tena Chelsea ikitaka saini ya kiungo N'Golo Kante.

Baada ya Zidane kuinasa saini ya Eden Hazard kwa ada ya pauni 130 m kutoka Chelsea pia alimtaka kiungo huyo lakini mipango ikabuma katika usajili uliopita.

Kuelekea kwenye usajili wa Januari tayari mipango ya kumsajili inaendelea kwa kuwa Zidane amekuwa na mipango mirefu na nyota huyo raia wa Ufaransa.

Kante mwenye umri wa miaka 28 aliwahi kukiri kuwania na Madrid na PSG bado ana mkataba wa miaka minne kuendelea kuitumikia Chelsea na analipwa pauni 290,000 kwa wiki.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic