September 13, 2019


Kocha wa Polisi Tanzania, Selemani Matola amefunguka kuwa mashabiki wa timu zote Tanzania ikiwemo Simba wanatakiwa kuzisapoti Yanga na Azam FC kwa kuwa zinawakilisha taifa na kuna faida ya kufanya hivyo.

Kauli hiyo imekuja baada ya Simba kufanya vizuri msimu uliopita kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika kwa kufika hatua ya robo fainali jambo lililosababisha timu nne za Tanzania kushiriki michuano ya kimataifa.

Msimu huu katika mashindano ya kimataifa, iliwakilishwa na Simba, KMC, Azam FC pamoja na Yanga,

Simba na KMC wametolewa tayari huku Yanga itacheza dhidi ya Zesco United ya Zambia kesho Jumamosi huku Azam FC ikiivaa Triangle United, Jumapili katika Uwanja wa Azam Complex, Chamazi.

“Unajua Yanga na Azam wanahitaji sapoti kutoka kwa Watanzania hasa wanapocheza hapa nyumbani, tunatakiwa kuwa kitu kimoja na kuweka kando mambo ya Simba, Namungo sijui Mtibwa, tuachane nayo kwanza kwa sasa tuwasapoti wenzetu.

“Kama tukisimama kuwaunga mkono Yanga na Azam hii ina faida kwetu kama nchini. Lakini pia wanatakiwa kutumia vizuri viwanja vya nyumbani na kutorudia makosa yale ambayo yalifanywa na Simba na KMC,” alisema Matola ambaye aliwahi kuwa Kocha Msaidizi wa Simba.

5 COMMENTS:

  1. Uwa nasema vichwa vya habarivya kuuza habari wakati habari yenyewe ni tofauti zinafanya blog yenu idharauliwe na mwandishi kuonekana wa ovyo! Matola ni kocha wa simba? Mnapenda sana kuuza habari kwa kutumia jina la simba "oh mchazaji wa simba" kumbe ni mchezaji wa zanani. Àcheni huo upuuzi

    ReplyDelete
  2. kama ni ishu ya kuwaunga mkono tu basi wameshapita. Tatizo ni performance uwanjani. Hivi vitu haviitaji maneno mengi. Huo mtazamo wa kutumia vizuri uwanja wa nyumbani ni kuficha udhaifu wa timu. Timu inatakiwa kucheza vizuri suala la kuungwa mkono baadae. Tatizo la timu zetu hakuna plan B.

    ReplyDelete
  3. Kichwa cha habari na habari kwa ujumla vinamtia aibu mwandishi na blog kwa ujumla.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic