LEO Simba
inatupa kete yake ya pili kucheza na Mtibwa Sugar na ilikuwa ikifanya
mazoezi yake Viwanja vya Gymkhana pamoja na jana uwanja wa Uhuru ilikuwa ni mazoezi ya mwisho.
Leo kutakuwa na sapraizi kubwa kwa Mtibwa Sugar kutokana na sura nyingi za kazi
kupewa nafasi ya kuanza kutokana na mazoezi ambayo Kocha Mkuu, Patrick Aussems
aliwapigisha vijana wake.
Kwenye
mchezo huo mpaka sasa inaonekana kwamba Aussems atapangua kikosi kitakachoivaa
Mtibwa ambapo kwenye vikosi viwili vya alivyotumia kikosi cha kwanza
kilikuwa kinaundwa na Aishi Manula ambaye ni mlinda mlango na upande wa mabeki
ilikuwa ni Erasto Nyoni, Mohamed Hussein, Yusuph Mlipili, Shomari Kapombe, Fraga Vieira, kwa
upande wa viungo ni Mzamiru Yassin, Hassan Dilunga, Clatous
Chama, Shiboub na mshambuliaji alikuwa ni Miraji Athuman.
Kwa upande
wa kikosi cha pili kiliundwa na Beno Kakolanya ambaye alikuwa ni mlinda mlango
kwa upande wa mabeki Pascal Wawa, Haruna Shamte, Kennedy Juma na Gadiel Michael
upande wa viungo wakiwa ni Jonas Mkude, Said Ndemla, Ibrahim Ajibu, Francis
Kahata na kwa upande wa washambuliaji ikiwa ni Deo Kanda na Rashid Juma.
Mwishoni
baada ya dakika tisini alimfanyia mabadiliko Jonas Mkude na Fraga Vieira,
Tshablala alichukua nafasi ya Gadiel.
Sura mpya ambazo huenda zikaonekana leo ni pamoja na Rashid Juma, Said Ndemla, Haruna Shamte, Kenedy Juma na Yusuph Mlipili ambao wamekuwa hawapati nafasi mara kwa mara ndani ya Simba.
0 COMMENTS:
Post a Comment