Dak ya 90, Goooooooli, Moliiiinga, anaisawazishia Yanga, sasa ni 1-1.
Dak ya 89, Hali bado mbaya kwa Yanga, bado wapo nyuma kwa ba0 1-0 wakati Yanga wakiwa pungufu.
Dak ya 86, Amos Makai anachukua nafasi ya Kipanga aliyeumia.
Dak ya 80, Hatari pale Molinga anakosa yeye na lango kwa kupiga kichwa mpira na unapaa juu ya lango.
Dak ya 77, Pamba wanapata kona, anaenda kupiga Mwaikimba, inapigwa na inakuwa goliki.
Dak ya 76, Ally Ally anapewa kadi ya njani kwa kufanya madhambi.
Dak ya 74, Gaudence Mwaikimba anaingia kuchukua nafasi ya Chidiebele Absalum.
Dak ya 73, Anaingia Maybin Kalengo kuchukua nafasi ya Ngassa, na sasa ni faulo, na kadi ya njano inatoka.
Dak ya 71, Faulo tena kwa Yanga, anapiga Molinga, piga paleee, kipa wa Pamba anadaka.
Dak ya 70, Pamba wanamiliki mpira eneo la kati, mpira unaenda kwa Chidebele, usharudishwa kwa Kabwili sasa na anaanza upya.
Dak ya 68, Kona inapatikana kwa Yanga, ni ya 10 sasa, inapigwa pale na inamkuta Molinga, piga kichwa huku lakini inagonga mwamba.
Dak ya 66, Mwalami anapiga moja kwa guu la kushoto, inawakuta wachezaji wa Pamba wanaukoa.
Dak ya 66, Mwalami anapiga faulo kushoto mwa uwanja, bado Mwamuzi hajaruhusu.
Dak ya 64, Inapigwa vizuri kwa guu la kushoto, Kabwili anapangua na Yanga wanapiga mpira mbele.
Dak ya 63, Pamba wanapata faulo karibu na aneo la hatari, kama wakitulia wanawe ongeza bao lingine, bado mpira umesimama.
Dak ya 60, Yanga wanaonekana kukosa umakini haswa katika eneo la ushambuliaji huku Pamba nao wakijaribu kulinda bao lao.
Dak ya 59, Toto anapokea pasi maridhawa kutoka kwa Molinga, mawasiliano yanakuwa si mazuri, Papmba wanaokoa.
Dak ya 59, Muharami Issa anaingia kuchukua nafasi ya Ali Mtoni kwa upande wa Yanga.
Dak ya 56, Rashid Njete ameingia kuchukua nafasi ya Nizar Khalfan kwa upande wa Pamba.
Dak ya 55, Yanga wanapata kona nyingine baada ya kipa Pamba, Kamene kutoa mpira nje akiokoa shuti kali, amepiga kona Ngassa lakini Pamba wanaokoa.
Dak ya 53, yanga wanafanya mabadiliko, anatoka Juma Balinya, Deus Kaseke anachukua nafasi yake.
Dak ya 51, Yanga wanapata kona ya saba, inapigwa lakini inakuwa ni offside.
Dak ya 49, Molinga anaotea, mshika kibendera kulia mwa uwanja ananyooosha kibendera juu, mpaka sasa Yanga wana kona sita.
Dak ya 46, Kipindi cha pili kimeanza kwa Yanga kushambulia kwa kasi lango la Pamba.
MAPUMZIKO: PAMBA SC 1-0 YANGA SC
Dak ya 45, Dakika moja imeongezwa.
Dak ya 45, Yanga bado wanahaha kupata bao la kusawazisha, mambo ni magumu.
Dak ya 38, Urikhob yawezekana si bahati yake leo, anapata jaribio jingine na mpira unakwenda nje.
Dak ya 36, Hamis Thabit anapewa kadi nyekundu kwa kumsukuma chini Fei Toto.
Dak ya 34, Faulo inapigwa kuelekezwa Pamba, Molingaaaaa, kipa Kameni anapangua na inakuwa kona, kona ya tatu kwa Yanga mpaka sasa.
Dak ya 30, Goooli, Pamba wanapata bao la kwanza kupitia kwa Saad Kipanga, boonge moja la bao.
Dak ya 29, Pamba sasa wanaenda langoni mwa Yanga, mpira anao Nizar Khalfan, pigwa kule golikiki.
Dak ya 26, Kona ya pili kwa Yanga, inapigwa lakini wachezaji wa Yanga wanajichanganya kwa kubabatizana kumalizia kambani, unaokolewa na mabeki wa Pamba.
Dak ya 23, Balinya naye anapata nafasi nyingine nje kidooogo ya eneo la 18 lakini mabeki Pamba wanaingia vema na kipa anadaka kuiulaiiini.
Dak ya 22, Urikhob anapata nafasi nzuri akiwa yeye na kipa ili kufumania nyavu, asalalee, mpira unaenda nje.
Dak ya 21, Lamine Moro anadondoka anaenda kugangwa nje ya uwanja, mpira umesimama.
Dak ya 17, Balama anashindwa kuuwahi mpira na kupasia kambani, mabeki Pamba wanautoa nje, inakuwa kona, pigwa pale, golikiki.
Dak ya 15, Moro anafanya madhambi pembeni kulia mwa uwanja kwa mchezaji wa Pamba, inakuwa faulo, pigwa pale, hatari!! Kabwili anadaka.
Dak ya 14, Balinya anapata nafasi nzuri ya kutumia kupiga shuti lakini mambo yanakwenda ndivyo sivyo.
Dak ya 13, Tshishimbi ameondondoshwa chini na wachezaji pamba, inakuwa faulo, mpira unapigwa kuelekea Pamba.
Dak ya 12, Pamba wanapata kona ya kwanza, inapigwa lakini inashindwa kuzaa matunda, golikiki.
Dak ya 8, Ngassa anapata nafasi nzuri ya kupiga shuti lakini linakuwa halina kipimo kizuri.
Dak ya 7, Tshishimbi anafanyiwa faulo na mpira unapigwa kuelekezwa Pamba.
Dak ya 5, Bado timu zote hazijaonesha ukomavu uwanjani.
Dak ya 4, Kocha wa Pamba anaonekana kutoa hamasa kwa wachezaji wake.
Dak ya 3, Kabwili ameanza leo, anawaanzishia wenzake kuanzisha mashambulizi upya, ni baada ya kuwa golikiki.
Dak ya 1, Pamba wamefanya shambulizi la hatari langoni mwa Yanga lakini wanajichanganya na mpira unatoka nje.
Dak ya 1, mechi imeanza baina ya Yanga dhidi ya Pamba, Uwanja wa CCM kirumba jijini Mwanza.








Jamaani mnatuumiza sisi wananchi
ReplyDeleteNi TFF ndo wamepanga ratiba mbaya kwa yanga naona wachezaji wamechoka
ReplyDeleteMsipojirekebisha viboko vinawasubirini
ReplyDeleteKiwango cha Yanga Ni cha Hali ya juu kabisa na naamini huu Ni mwaka WA yanga kukumba makombe yote juu ya maoneo ya marefa. Yanga Oyeee
ReplyDeleteHayo ndio matokeo ya mabilioni na Zesco watalala tu Landumina ataaibika tu. Asanteni watoto WA Jangwani
ReplyDeleteMungu ainusuru yanga na kikosi chake cha maangamizi. Ikiwa mambo ni hayo, Kwa Zesco tutaraji nini
ReplyDeleteMiamba yatoka droo
ReplyDeleteSioni sitambui kama kocha wa yanga ataendelea kutwambia bado anaunganisha timu. Hapa achukue hatua za kuwajibika mwenyewe na ameshindwa.
ReplyDeleteEti Kwa muda WA wiki mbili anawsfundisha namna ya kutia magoli na mwisho WA wiki mbili matokeo ndio yale tuliyoyaona. Aibu tupu na huku malumbano ya kikaputura cha Zahera kikishika Moto Kwa chalenji za hapa na pale na huku timu ikikosa msimamo haonekani Balinya wala badala WA Makambo aliyepigwa bei
ReplyDelete