TANZANIA inapenya hatua ya makundi leo kwa ushindi wa penalti 3-0 dhidi ya Burundi mchezo wa kufuzu Kombe la Dunia mwaka 2022 nchini Qatar.
Dakika 90 zilikamilika kwa timu zote kufungana bao 1-1 kisha zikaongezwa 30 ngoma ikawa sare kwa timu zote mbili.
Mpaka dakika 120 zinakamilika ngoma ilikuwa ni 1-1 jambo lililopelekea mshindi kupatikana kwa njia ya mikwaju ya penalti.
Kwa upande wa Tanzania bao la kwanza lilifungwa na Mbwana Samatta dakika ya 29 na likasawazishwa na Abdul Fieston dakika ya 45.
Kwenye changamoto ya Penalti Erasto Nyoni alipachika ya kwanza ya pili Himid Mao na ya tatu Gadiel Michael.
Kaseja alipangua penalti moja na mbili wapigaji wa Burundi walikosa.
0 COMMENTS:
Post a Comment