September 17, 2019


Aliyekuwa Mwenyekiti wa Baraza la Wadhamini katika klabu ya Simba, Hamis Kilomoni, amemtaka Mkuu wa Bodi ya Wakurugenzi, Mohammed Dewji 'Mo' kuweka bilioni 20 katika akaunti ya klabu hiyo.

Kilomoni ameibuka na kauli hiyo baada ya Mo kushindwa kuweka fedha hizo hadi sasa ili ziweze kutumika ndani ya klabu kwa mambo mbalimbali.

Ameeleza anashangwaza na Mo kama ameamua kuwekeza kwanini asiweke fedha hizo kama kweli amewekeza na siku zinazidi kwenda.

Amefunguka akieleza kuwa yeye si kwamba anapinga Mo kufanya uwekezaji bali ni vema taratibu zote akazifuata na si kuitumia Simba kwa manufaa yake pekee.

"Ujue mimi nashangaa mpaka leo Mo hajaweka zile bilioni 20 alizoahidi mpaka leo.

"Nashangaa amekuwa kimya, kama amewekeza kwanini asiziweke kwenye akaunti ya klabu, ni uwekezaji gani huo?

"Mimi sipindi yeye kufanya uwekezaji, ninachotaka ni vema akafuata tu taratibu zinazototakiwa na kila mtu atamuunga mkono."

16 COMMENTS:

  1. Anamsubiri manara aseme yes Mzee we can do it

    ReplyDelete
  2. Mwandishi kabla huja andika upuuzi wowote ambao utakufanya uonekane kanjanja fuatilia mambo yanaendaje labda kama una lengo vingine,soma maagizo ya waziri kuhusu utengenezaji wa kanuni za uwekezaji

    ReplyDelete
  3. Kwani mabilioni yanayotumika Kwa kuiendesha Simba hata ikafika ilipofikia ambapo katika tarehe yetu ya kimpira wetu hapana timu yeyote iliyofika gharana zote hizo Nani anayezitoa ambapo hatujasikia malalamiko kuwa wachezaji hawajalipwa haki zao au matakwa ya ya Baraza la ufundi hayajatekekezwa au Simba ina madeni? Ni juu yetu kushukuru Ile wakati Simba alipokuwa mnyonge na pale waliokuwa na hela wakati ule jinsi walivoinyanyasa Simba Kwa kumchukuwa kila mchezaji wanaemtaka he hayo yapo sasa. Simba haitaki yatokee tena pale hela ya Simba ilipotoweka wakati ikisadikiwa ipo benki

    ReplyDelete
  4. Muheshimiwa Magufuli amesema wapinzani watakuwepo ila ni sawa na kelele za chura kwenye maji kamwe haziwezi kumzuia ng'ombe kunywa maji.Mzee kilomoni ni sawa na chura mpiga kelele kwenye maji kamwe hawezi kuzuia watu kufanya shughuli zao. Hapa utaona yakuwa Mwandishi ni kilaza na ni ushuzi mtupu. Tena ni ushuzi wa mtu mzima hata nguvu hauna unabakia kunuka tu.Watanzania wengi wameshamuelewa Magufuli yakwamba watanzania tunatakiwa kufanya nini hivi sasa. Ni kukasirika katika kutafuta maendeleo piga ua lakini wakati wengi wa watanzania wakiwa wametamalaki kuchangamkia kuleta maendeleo nchini lakini bado kuna kundi la watanzania wenye kufanya jitihada za dhati na za makusudi kabisa za kifisadi kukwamisha juhudi za waleta maendeleo nchini. Hawa tukiwachekea basi tunajijengea mazingira ya kuja kujuta na kulia kama wafiwa.Tukirudi nyuma ni majuzi tu utaona ni waandishi wetu wenyewe waliosherehesha kelele za watanzania waliofurahi baada ya ndege yetu kukamatwa kule Africa kusini.
    Leo hii utaona Mtu anaejifanya wa kutaka kuona maendeleo ya michezo nchini hasa mpira wa miguu yakija juu kama Salehe Jemebe kashikilia upuuzi wa kumsherehesha Kilomoni kila kukicha kwenye Blog zake.Mwakyembe alikwenda Bunju nakusema ule mradi wa kule Bunju ni kiboko kiasi cha kuahangaa Simba jeuri ya kufanya mambo makubwa kama yale wanaipata wapi?
    Magufuli alimuwasa Mo kamwe asivunjike moyo na baadhi ya vikwazo anavyokutana navyo katika uwekezaji nchini.
    Waziri mkuu anaviomba vilabu vyengine kufuata nyayo za Simba katika kujikomboa kiuchumi ila waandishi wetu hawaoni cha kuandika zidi ya Simba isipokuwa upuuzi wa kilomoni kutaka kuirejesha Simba katika hali ya omba omba kama si mapepo ya hovyo katika vichwa vya baadhi ya watanzania kitu gani?

    ReplyDelete
  5. Mimi nadhani kama Mzee Kilomoni yuko sahihi. Kama makubaliano kama mwekezaji kuweka 20 billioni na iko kwenye maandishi na muda wa kuziweka ni kwa nini hizo hela zisiwekwe?.

    ReplyDelete
    Replies
    1. MO atawekaje bilioni 20 ikiwa taratibu na kanuni hazijakamilika?Kwani Kilomoni ni mmoja wa wajumbe kwenye bodi?Ni Bora mchakato uende taratibu kuliko pesa zitumbukizwe bank ziishie kunyofolewa Kwa malipo hewa.Kwa nini hatujifunzi Kwa viongozi wetu walio na kesi?Hivi Kilomoni ana ajenda gani ni 20bilion za za mwekezaji? Majuz Kati huyu Kilomoni na wazee wenzake walidai MO hafuati taratibu sababu wanatakiwa wawekazaji zaidi ya watatu kwa mujibu wa kanuni za uwekazaji hisa. Leo hii mzee Kilomoni anaibuka na kudai Kwa nini MO haweki 20b bank? ili zifanyie nini??? MO alishatoa mchanganuo wa hizo 20B na alieleza wazi Kwa waandishi wa habari kuna process hazijakamilika. Ni mwenyekiti Nkwabi aliyepaswa kuitisha mkutano wa wanachama waliyemchagua kutueleza kinachoendelea tokea wanachama wabariki mfumo wa mabadiliko ya klabu.Hata mwaka haujaisha mwenyekiti anatukimbia Kwa hoja dhaifu.kama alijua atabanwa na shughuli zake basi ni Kwa
      nini hakufanya kama Ramadhani Mtemi ambaye alijitoa mapema kabla ya uchaguzi?Aelewe Nkwabi ametupotezea muda wetu kukesha kumpigia Kura siku anaIle.Ni wazi Nkwabi kajiuzulu kwa pressure ya mzee Kilomoni na kundi lake.Kwani wanachama wa Simba ni mzee Kilomoni tu? Hawa wazee conservative wanarudi tena kuivuruga Simba kama walivyofanya 1976 walipoondoka Simba na kwenda kuanzisha klabu iliyoitwa 'Nyota Nyekundu'wakijiita Sunderland original.Sielewi Kwa nini walirudishwa Simba na sasa wanachochea migogoro isiyo na tija.

      Delete
  6. Hofu Ni kuwa zitatoka Kwa njia ya Panya

    ReplyDelete
  7. Kuna taratibu za kufuatwa na Bodi ya Simba inajua hilo. Nashangaa kwanini mwandishi hakutaka kuifuatilia zaidi hii stori. Mimi nilidhani mwandishi badala ya kukurupuka kuandika alichosema Kilomoni ange-balance stori yake kwa kuwatafuta viongozi wa Simba na hata MO mwenyewe. Huo ndio uandishi wa habari wenye weledi. Kinyume cha hapo ni UKANJANJA tu.

    ReplyDelete
  8. Mimi nahisi kama mzee Kilomoni ni mgonjwa wa akili kama wale wanaohisi kuwa yupo sahii kwani kuhoji kitu ambacho tayari kilishaingiwa mikataba ya kimaandishi katika hali ya uwazi na ipo katika utekelezaji ni dalili ya kuchanganyikiwa kwa mwenye kuhoji.Tanzania ya Magufuli sio awamu ya ubabaishaji na kama Kilomoni alizoea kupiga Simba huko nyuma basi hizo billioni 20 atazisikia hewani tu.

    ReplyDelete
  9. Anataka akabdfhiwe yeye azihifadhi

    ReplyDelete
  10. Hakika kuna kitu fulani anataka kucheza mzee kilomoni na pesa ya uwekezaji. Kazua waraka kwa matarajio ya kupewa kiwachia waraka. Mzee na wale wapambe wake wanaomshauri wanataka kumtia mjini Mo ila Mo ameshamshtukia. Mara waraka or mara billioni 20 kwani yeye ndio muhasibu wa Simba?

    ReplyDelete
  11. Kunguru kasema binaadamu hana kibyongo na ukimuona na kibyongo basi Kuna lake anataka kulitenda. Hizo bilioni ishirini zimemrusha akili na kumnyima usingizi na huku mate yakimtoka. Fisi anapomuona MTU akipunga mkono humfata Kwa tamaa mkono udondoke aupate yeye. Hatutaki kuiona hela ya Simba ikivuja kama Ile hela ya mauzo ya Okwi n

    ReplyDelete
  12. Kwani huyo Kilomoni Kwa sasa Ni Nani Kwa Simba au ndio anajirejesha awe keshia. Hahaa kachelewa ndio katuwa juu ya Paa Kwa ungo

    ReplyDelete
  13. Huyu Mzee aseme hayo mambo ambayo hiyo pesa inataka kufanya ni mambo gani,sio mafumbo yake ya kipuuzi

    ReplyDelete
  14. Huyu Mzee aseme hayo mambo ambayo hiyo pesa inataka kufanya ni mambo gani,sio mafumbo yake ya kipuuzi

    ReplyDelete
  15. Daa Kweli Bora Kukaa Kimya Kuriko Kuropoka

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic