KUELEKEA hatua ya robo fainali ya michuano ya Sprite Bball Kings inayotarajiwa kuchezwa Jumapili ya wiki hii kwenye Uwanja wa Ndani wa Taifa jijini Dar es Salaam ni noma kweli kutokana na timu zote zilizotinga hatua hiyo kuwa tishio.
Michuano hiyo ambayo huu ni msimu wake wa tatu, hatua ya mtoano ilianza Agosti 25, mwaka huu kukiwa na zaidi ya timu 30 ambapo sasa zimebaki nane zikiisaka shilingi milioni 10 ambayo itakwenda kwa bingwa.
Goza Chuma ambaye ni Ofisa Habari wa michuano hiyo, ameitaja ratiba ya mechi za robo fainali zitakazochezwa Jumapili kuanzia saa 2 asubuhi ni Flying Dribblers Vs Dream Chasers, K.G Dallas Vs Water Institute, Tamaduni Vs Ukonga Hitmen na Mchenga Bball Stars Vs TMT.
"Hatua hii ya robo fainali itakuwa ni noma kweli kwani timu zote zilizotinga hapa si za kawaida, zote ni hatari, hivyo ushindani utakuwa mkubwa sana na sijui nusu fainali itakuwaje.
"Kwa kifupi kila hatua inayokwenda mambo yanakuwa matamu zaidi mashabiki ," amesema Chuma.
0 COMMENTS:
Post a Comment