UONGOZI wa Yanga umesema kuwa
itakuwa kazi ngumu kwa wapinzani wao Zesco kupenya uwanja wa Taifa kwani wamejipanga kumaliza mchezo mapema kutokana na hasira walizopewa na Simba pamoja na
KMC.
Akizungumza na Saleh Jembe,
Mratibu wa Yanga, Hafidh Saleh amesema kuwa kutolewa kwa Simba mapema licha ya
msimu uliopita kufanya vema kumewapa hasira ya kupambana ili kutinga hatua ya
makundi.
"Kwa sasa tunajua kwamba Simba
ameshatolewa kwenye michuano hii ya kimataifa pamoja na KMC kutolewa kwao
kumetufanya tuwe na hasira ya kupambana kutafuta matokeo chanya kwenye michezo
yetu.
" Kufanya kwetu vizuri
kutaongeza pointi na idadi ya timu shiriki tukishindwa itakuwa pigo, mashabiki
watupe sapoti nasi hatutawaangusha katika hilo kikubwa ni kuamini kwamba
tunaweza," amesema Saleh.
Yanga itamenyana na Zesco, Septemba
14 uwanja wa Taifa ikiwa ni mchezo wao wa hatua ya kwanza kwenye Ligi ya
Mabingwa Afrika.
Imeweza Pamba na Ruvu shooting na polisi kupenya ngome ya Yanga yenye mastaa WA kila aina ishindwe Zesto
ReplyDeleteNGOJA TUONE
ReplyDeleteRaha ni kufananisha mechi mazoezi na mechi halisi... mechi mazoezi huchezwa kutafuta mfumo na kutazama ufiti wa wachezaji... kabla ya kuandika tuangalie vikosi vilivyocheza mechi za kirafiki na zile za kimataifa.
ReplyDeleteHaya mazoezi kutafuta mfumo tutaona mpira wa mdomoni wa watanzania tulishazoea,mnaweza kushinda moja bila ukaenda Zambia kulowa siyo kufungwa kulowa
ReplyDelete