September 28, 2019


Yanga imeondolewa rasmi katika Ligi ya Mabingwa Afrika kwa kukubali kufungwa mabao 2-1 dhidi ya Zesco United.

Zesco ndiyo waliokuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa Jesser Were mnamo dakika ya 25 kabla ya Yanga kusawazisha kwenye dakika ya 31 kupitia kwa Sadney Urikhob.

Mpaka dakika 45 za kwanza zinamalizika Yanga na Zesco walikuwa na matokeo sawa ya 1-1.

Kipindi cha pili kilianza kwa timu zote kufanyiana mashambulizi kwa zamu na katika dakika ya 79, Abdulaziz Makame alijifunga na kuwapa Zesco bao la pili alipokuwa kwenye harakati za kuokoa mpira.

Mpaka dakika 90 zinamalizika, Yanga walikuwa nyuma kwa mabao 2-0 ambayo yamewafanya waondolewe kunako Ligi ya Mabingwa sa sasa watacheza Shirikisho Afrika.

Pia, katika mchezo huo, Lamine alipewa kadi nyekundu mnamo dakika ya 90 kwa kucheza mchezo usio wa kiungwana.

16 COMMENTS:

  1. Rejeeni nyumbani na mjitayarishe upwa. Kuanguka si kushindwa, kushindwa ni kubaki pale ulipoangukia

    ReplyDelete
  2. Wacha warudi. Kelele zingekuwa nyingi.Makundi my foot.

    ReplyDelete
  3. Kelele ohh tutapindua meza .Haya mmekuta mkeka utapinduaje?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mpira mliuangalia?au ndo mashabk wa kucoment stil wananchi wapo kwenye mashindano ya kimataifa wanarud confideration cup,safu ya ushambuliaj ikiwekwa sawa yanga bado timu nzur defense iko vzur
      Wababe wa zeemba haya kapgwa kwao 4 nyie mlisubir kumpiga taifa

      Delete
    2. Unamaanisha Yanga imecheza vizuri? Utakuwa ulikuwa unaangalia Yanga tu walipokuwa wanapata Mpira

      Delete
  4. Kombe la waliofungwa. Kupindua meza my foot.Timu inajihami mpaka mnajifunga wenyewe kwa kujaa golini.Mwingine kalimwa umeme.Mbeya City wanawasubiri.Kwa zawadi hiyo sijui mtamfunga nani.

    ReplyDelete
  5. Maskini Zahera sijui kama atapona safari hii

    ReplyDelete
  6. Kuna kuzidiwa na kuna bahati, kwa siku ya leo yanga hawakua na lolote kati ya hayo mawili na ndiomana wakajifunga, tuwaombee warudi shirikisho kwa nguvu na wakafanye vizuri.

    ReplyDelete
  7. Meza imewapindua chali walooazimia kupinduwa Rudini tutakuja kukupokeeni kishujaa

    ReplyDelete
  8. Ukisikia mwanaume kafia vitani ndo hii ya yanga, Ila mama kafia jikoni ndo ile ya ud songo

    ReplyDelete
    Replies
    1. kweli vitani kwa kujitwanga risasa mwenyewe!kulikuwa na haja ya kwenda Zambia?

      Delete
  9. Kufungwa na kutolewa kwa kanuni ya magoli kuna tofauti.Aliyefungwa anajulikana. Tena alienda kwa fadhila ya mume anajulikana.Wacheni ngebe Mbeya City wanawasubiri. Ruvu Shooting walishafanya yao.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Lakini pia kuna tofauti ya kati ya kutolewa hatua ya awali na hatua aliotolewa mnyama.

      Delete
    2. kujitoa mwenyewe kwa kujifunga?Acheni zenu..Eti taa zilizimwa kwani zesco wao ni paka wanaona gizani

      Delete
  10. Sima's Glorious death was better than......

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic