September 28, 2019


MOTO wa Liverpool ndani ya Ligi Kuu England umezidi kuwaka leo baada ya kushinda kwa mbinde mbele ya Sheffield United.

Liverpool ilipata bao la ushindi dakika ya 70 kupitia kwa Georginio Wiljnaldum's na kuifanya izidi kujikita kileleni kwa ushindi wa bao 1-0.

Leo kikosi hicho kimefanya kazi ngumu kupata pointi tatu kwani Sheffield walikuwa wasumbufu mwanzo mwisho uwanjani.

Beki kisiki, Virgil Van Dijk na Joel Matip hawakuwa nyuma kulinda lango lao kwani waliweka ukuta wa jiwe langoni mwao.

Huu ni ushindi wa 7 mfulululizo kwa Liverpool ndani ya EPL na imefunga jumla ya mabao 18 ikiwa na pointi 21.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic