October 8, 2019

Beki wa Simba Kennedy Wilson (kushoto) akiwa na Ripota wa Saleh Jembe, George Mganga.

Na George Mganga

Beki wa timu ya Simba, Kennedy Wilson, amesema siku moja anatamani kuichezea timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars.

Kauli ya beki huyo imekuja kipindi hiki ambacho Stars ipo kwenye nafasi ya kuwania kucheza mashindano ya CHAN ambayo yatakayofanyika nchini Cameroon mwaka kesho.

Wilson ameeleza kuwa na ndoto hiyo kwani amekuwa akiitamani kwa muda mrefu tangu anaanza kucheza soka enzi za utoto wake.

Wilson ambaye kabla ya kujiunga na Simba, amefunguka kwa kusema juhudi na kupambana ndani ya timu yake ndiyo njia pekee itakayoweza kumpa nafasi ya kucheza Stars.

Ameeleza kuwa ni ngumu kuitwa ukiwa haujafanya chochote ndani ya klabu, bali inapaswa kupambana ili kumshawishi kocha ambaye akikuona unafaa, anaweza akakuita kikosini.

"Kiukweli natamani kuichezea Stars sababu ni ndoto zangu tangu nikiwa mdogo, kinachotakiwa ni kupambana na kuonesha jitihada mazoezini ili kocha aniite.

"Mungu ni mwema, naamini ndoto hii itatimia kama imepangwa ila nitazidi kujituma zaidi nikiwa na timu yangu ya Simba malengo yaweze kutimia."

Tangu atue Simba akitokea Singida United, Wilson amecheza mechi moja pekee ya Ligi Kuu dhidi ya Biashara United waliyoshinda mabao 2-0 huko Musoma, Mara.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic