October 2, 2019


Baada ya kuondolewa kwenye raundi ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika, Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera ameanika mipango yake mipya kuelekea Kombe la Shirikisho Afrika.

Yanga itashiriki kombe hilo baada ya kuondolewa na Zesco United ya Zambia katika baada ya kufungwa wikiendi iliyopita mabao 2-1 mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa Levy Mwanawasa na hivyo kutolewa kwa mabao 3-2.

Yanga hivi sasa inasubiria kuchezwa kwa droo ya Shirikisho la Soka Afrika (Caf) itakayochezeshwa wiki ijayo ili kujua atacheza na nani.

Zahera alisema amejifunza mengi katika ushiriki wa michuano hiyo na kitu walichokosea ni kucheza bila mipango ya ushindi wa mabao mengi nyumbani.

Zahera alisema ushindi wa mabao mengi kuanzia matatu wa nyumbani ni mtaji mkubwa watakapokwenda ugenini, hivyo amejipanga kuhakikisha makosa waliyoyafanya kwenye Ligi ya Mabingwa hawayafanyi kwenye shirikisho.

“Hili kuwa na uhakika wa kutinga makundi tunahitaji kufunga mabao mengi nyumbani, tutaanzia hapa kabla ya kwenda kurudiana na wapinzani kwao.

“Huo ndiyo mpango mkakati niliopanga kuuanza katika Shirikisho, kwani tayari benchi la ufundi pamoja na wachezaji tumejifunza hilo, unapokuwa na mtaji mkubwa wa mabao ukiwa nyumbani, basi ni rahisi kufuzu ugenini kutokana na presha itakayokuwepo kwa wapinzani wetu.

“KiuKweli tulikuwa na changamoto kubwa kwenye safu yetu ya ushambuliaji ambayo ilikosa umakini katika umaliziaji kutokana na kutengenezewa nafasi nyingi na kushindwa kuzitumia, lakini sasa nadhani tumeanza kuwa vizuri.

“Hatupaswi kurudia makosa tuliyofanya Ligi ya Mabingwa, tunahitaji kufunga mabao zaidi ya mawili tukiwa nyumbani ili kupunguza presha ya mchezo wa ugenini na hilo linawekana kwetu,” alisema Zahera.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic