October 11, 2019


IKIWA inajinoa kwa ajili ya mchezo wake dhidi ya Simba utakaopigwa Octoba 23 uwanja wa Uhuru tayari mashine yake ya kazi imerejea kuanza mazoezi na timu kwa sasa.

Nahodha wa Azam FC, Agrey Moris, tayari amerejea mazoezini akitokea kwenye majeruhi aliyokuwa akiyauguza nchini Afrika Kusini.

Moris alipata maumivu ya goti, Juni mwaka huu, kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya timu ya Taifa ya Misri, wakati akiwa na kikosi cha Tanzania 'Taifa Stars' iliyokuwa ikijiandaa na fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON) zilizofanyika Misri.


Azam FC imecheza jumla ya michezo mitatu mpaka sasa na haijapoteza mchezo hata mmoja huku ikifungwa bao moja na Namungo FC na yenyewe ikifunga jumla ya mabao matano.

Itashuka uwanjani kucheza mchezo wake wa nne na Simba ambao ni mabingwa watetezi wa ligi msimu huu.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic