October 11, 2019


Kocha Msaidizi wa Mashujaa FC, Kajembe Abdallah ambaye atakutna na Simba katika mchezo wa kirafiki, amefungiwa mechi tatu na kutozwa faini ya sh. 300,000 (laki tatu) kwa kutolewa katika benchi kwa kadi nyekundu baada ya kumtukana Mwamuzi Msaidizi. 

Adhabu ni kwa mujibu wa Kanuni ya 41(11) ya Ligi Daraja la Kwanza kuhusu Udhibiti kwa Makocha.

Mechi namba 9B: Gwambina FC 1 v Stand United 0– Kamishna Nestory Matiku amepewa Onyo kwa kutoa taarifa isiyojitosheleza ya mechi hiyo iliyochezwa Septemba 21, 2019 katika Uwanja wa Gwambina mkoani Mwanza.

Mechi namba 10B: Geita Gold FC 1 v Rhino Rangers 0- Meneja wa Rhino Rangers, Ali Rhumba amepelekwa Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) baada ya kumpiga Mwamuzi Msaidizi Omari Mataka na kumjeruhi chini ya jicho katika mechi hiyo iliyofanyika Septemba 21, 2019 kwenye Uwanja wa Nyankumbu mjini Geita.

Nao wachezaji wa Rhino Rangers (Simon Joseph Kiula juzi no. 5 na Julius Elias Masunga jezi no. 26) wanapelekwa Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kwa kuwarushia mawe waamuzi baada ya kumalizika mechi hiyo. 

Polisi waliokuwa uwanjani walijitahidi kupambana na licha ya kupata upinzani kutoka kwa wanajeshi kadhaa waliombatana na Rhino Rangers.

Mechi namba 12B: Sahare All Stars 1 v Green Warriors 1- Kipa wa Green Warriors, Shabani Dihile amepewa Onyo Kali kwa kutoa shutuma dhidi ya waamuzi kuwa walichezesha kwa maelekezo ya viongozi mechi hiyo iliyochezwa Septemba 22, 2019 katika Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga. 

Adhabu ni kwa mujibu wa Kanuni ya 14(49) ya Ligi Daraja la Kwanza kuhusu Taratibu za Mchezo.

Mechi namba 13B: Stand United 3 v Green Warriors 2- Klabu ya Green Warriors imetozwa faini y ash. 200,000 (laki mbili) baada ya wachezaji wake kuingia uwanjani kwa kutumia mlango usio rasmi katika mchezo huo uliofanyika Septemba 27, 2019 Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga. 

Adhabu ni kwa mujibu wa Kanuni ya 14(49) ya Ligi Daraja la Kwanza kuhusu Taratibu za Mchezo.

Mechi namba 17B: Pamba SC 1 v Geita Gold FC 2- Meneja wa Pamba SC, Jafari Juma amepelekwa Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) baada kwa kumpiga ngumi Mwamuzi, tukio lililosababisha askari polisi wamweke chini ya ulinzi katika mechi hiyo iliyofanyika Septemba 28, 2019 kwenye Uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic