October 2, 2019


Bosi mkuu wa benchi la ufundi la Simba, Mbelgiji, Patrick Aussems amewaambia viungo wake wawili Ibrahim Ajibu na Said Ndemla kuwa wasiwe na wasi juu ya namba kwani watacheza sana msimu huu.

Viungo hao wawili mwanzoni mwa ligi hawakuwa na nafasi kubwa ya kuwemo kwenye kikosi cha kwanza lakini kikosi hicho kiliposaļ¬ ri kuelekea Kanda ya Ziwa kucheza na Kagera Sugar na Biashara United walitumika na kuwemo sehemu ya Simba kutwaa pointi sita kwenye mechi hizo mbili.

Viungo hao walianza sambamba kwenye mechi na Biashara United ambapo Ajibu alitoa asisti moja kwa Miraji Athuman ‘Sheva’ na kuifanya Simba kushinda mabao 2-0 kwenye mechi hiyo iliyopigwa Jumapili iliyopita mkoani Mara.

Aussems amesema kuwa amefurahishwa na uwezo wa viungo wake hao wawili kwenye mechi hizo lakini atawatumia zaidi katika michezo mingine kutokana na mipango yake.

“Siyo Ajibu na Ndemla pekee ambao wamefanya vizuri katika mechi tulizocheza kule Kanda ya Ziwa bali wachezaji wote wamefanya vizuri, ila wao nawapongeza kwa kile ambacho wamekionyesha.

“Kuhusu suala la kucheza, hapa nina wachezaji wengi ambao nimewasajili kwa ajili ya ligi kwa hiyo ni lazima kila mmoja aweze kupata nafasi ya kucheza. Kila mmoja ana nafasi yake na utaona anacheza kwenye mechi fulani, nitabadili timu kwa kuangalia mechi yetu inataka wachezaji wa namna gani,” aliweka wazi kocha huyo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic